HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 7, 2016

WATEJA WA DCB KUNUFAIKA NA KAMPENI ZA BORESHA MAISHA NA PATA FAIDA

Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya boresha maisha na DCB pamoja na Pata faida na DCB itakayoanza kuchezwa kwa droo ya kwanza Desmba 17, Kushoto ni Meneja Masoko Boyd Mwaisame.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BENKI ya DCB imedhamiria kuendelea kuwa kuwajali wateja wake imeanzisha kampeni ya "boresha maisha na DCB" na " Pata faida na DCB" itakayoanza Desemba 17 kwa ajili ya kuwazawadia zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kwa wateja wapya na wa zamni.

Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo amesema kampeni boesha maisha na DCB na Pata faida na DCB itadumu kwa miezi mitatu na kila mwezi kutakuwa na droo moja itakayotoa washindi watatu wa fedha taslimu laki mbili,

Dyamo amesema kuwa mbali na fedha taslimu kutakuwa na washindi wengine wawili watakaopata simu za mkononi na washindi 20 watapata kila mmoja na watatangazwa mbele ya waandishi wa habari na kukabidhiwa zawadi zao.

Droo ya kwanza itachezeshwa Desemba 17 na itamalizika Februri 17 na wateja wanatakiwa kuweka fedha mara kwa mara kwenye akaunti mojawapo ya akiba binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI kiasi cha kuanzia sh 50,000 na kuendelea na kuongeza amana mara mbili zaidi ya sh 500,000.

Dyamo amesema kuwa, mteja atakayeweka fedha hizo ataingia moja kwa moja kwenye droo hizo, mbali na kampeni hiyo pia kutakuwa na kutakuwa na Pata faida na DCB itakayokuwa inawapa faida wateja kwa kuwekeza nkupitia huduma yetu ya akaunti ya muda mrefu (fixed account) kwa kuweka kiais cha milioni 50 na kuendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja na watapata faida ya asilimia 15 ya fedha zako.

Alisisitiza kuwa, hata kama utaziweka fedha zako kwa kipindi cha miezi sita bado utaendelea kufaidika zaidi na kuwataka kujitokeza kwa wingi hususani kwa wajasiramali, watu binafsi na taasisi mbalimbali.

Meneja wa matawi wa  DCB, Haika Machaku amewataka watanzania kujiunga na benki yao kwani asilimia kubwa ya faida inaenda kwa wananchi kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Meneja wa matawi wa  DCB, Haika Machaku akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na benki yao ili kuweza kufaidika zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad