HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2016

WATANZANIA WAPENDE KUNUNUA BIDHAA ZA NDANI KUIFANYA SEKTA YA VIWANDA IWEZE KUKU-DK. ADREHEM MERU

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema katika kuendeleza viwanda nchini  watanzania wanatakiwa kupenda kununua bidhaa za ndani ili kuifanya sekta ya viwanda ikue kwa kasi .

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru wakati wa kufunga maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema maonesho ya viwanda yamefungua njia katika kuelekea uchumi wa viwanda na kulifanya taifa kupata maendeleo na kazi hiyo waikufanya ni watanzania na mataifa mengine kuunga mkono uwekezaji wa viwanda.

Dk. Meru amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano na sekta binafsi katika kukabili changamoto sekta hiyo ikiwemo mitaji ya uanzishaji wa viwanda. 

Aidha amesema watanzania waache kutia doa juu ya wawekezaji hali ambayo itanya wengine washindwe kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka amesema watu wenye viwanda wameonyesha ushiriki na kuahidi maonesho yajayo yatafana. 

Rutageruka amesema watanzania wakipenda kununua bidhaa za ndani watafanya viwanda kuendelea kukua.

Maonesho hayo yameshirikisha viwanda vidogo 300 na viwanda vikubwa 96 taasisi za serikali 13 pamoja na taasisi za fedha Tano( 5).

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akizungumza katika ufungaji wa maonesho ya viwanda vya ndani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza na washiriki maonesho ya Viwanda jijini Dar es Salaam

Kikundi cha Sanaa cha watu wenye Ualbino wakitumbwiza wakati wa ufungaji maonesho ya Viwanda.

.Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akimkabidhi cheti cha udhamini wa maonesho ya viwanda,Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel jana katika 
viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam

 Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akimkabidhi cheti cha ushiriki maonesho ya viwanda, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza (ACP), Joel Bukuku jana katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akimkabidhi cheti cha ushiriki maonesho ya viwanda, Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji , Rosemary Mkandala jana katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akimkabidhi cheti cha ushiriki maonesho ya viwanda, Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi , Adella Kayella jana katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akipata maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda hilo jana 
katika maonesho ya viwanda vya ndani yaliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaaji-Viwanda, Dk. Adrehem Meru akipata maelezo kwa Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), James Ndege wakati alipotembelea banda hilo wa katika maonesho ya viwanda.
Sehemu washiriki wakiwa katika ukumbi kwa ufungaji wa maonesho ya viwanda vya ndani jana.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad