HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 9, 2016

WAAJIRI WATAKIWA KUWAPA WAFANYAKAZI WAO FURSA YA KUJIFUNZA ILI KUWAJENGA KIUWEZO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa amewataka waajiri kuendelea kuwapa fursa wafanyakazi wao kwa kwenda kupata ujuzi wa aina mbalimbali kwani serikali imeadhimia kutoa mafunzo mahsusi kwa lengo la kuwajenga uwezo waajiriwa.

Majaliwa amesema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka iliyoandaliwa na  Association of Tanzania Employer (ATE) zilizofanyika jana usiku na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.,

Katika utoaji wa tuzo hizo, Majaliwa amesema kuwa waajiri wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa upatikanaji wamitaji, tozo ya kuendeleza ujuzi na utiriri wa tozo mbalimbali ambapo huwa inawapa ugumu kuweza kuwapa stahiki waajiriwa na kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige amesema kuwa bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ila wanaimani kuwa kutokana na ushirikiano wanaoupata sasa hivi kutoka kwa serikali ya awamu ya tano wana uhakika wa kuweza kutimiza malengo ya waajiriwa ili kupata haki zao.

Maige amesema kuwa bado wataendelea kuandaa tuzo hizi na zaidi Ubalozi wa Norway umeonesha nia nzuri ya kushirikiana nasi kuweza kuona tunafikia makengo mazuri.

Mkampuni na mashirika mbalimbali waliweza kushiriki na kufanikisha hafla hiyo ikiwemoi NSSF, PPF, NHC, SSRA, Geita Gold Mine, Coca Cola, MeTL, ACACIA na mengine pia.

Mshindi wa kwanza wa tuzo ya mwajiri bora ni Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) wakifuatiwa na Coca cCola Kwanza na mshindi wa tatu ni Geita Gold Mine.
 Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wakati wa utoaji wa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 jhafla iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam, Kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.

 Tuzo mbalimbali zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kupatiw amakampuni yaliyoshiriki mwaka 2016.

Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employer (ATE).

Mwenyekiti wa Association of Tanzania Employer (ATE), Almas Maige akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza ya tuo ya mwajiri bora mwaka 2016 Afisa Mwajiri Mkuu wa Tanzania Breweries Limited (LTD) David Magese jana Jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa pili ya Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 Meneja  Mwajiri Coca Cola Kwanza Sigifrid Faustine jana Jijini Dar es salaam.


Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akitoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa shindano la mwajiri bora lililoandaliwa na Association of Tanzania Employers (ATE) lililofanyika jana Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka makampuni mbalimbali na washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka 2016 katika vuipengele tofauti.
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Picha zote na Zainab Nyamka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad