Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KUFUATIA Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka Wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ wasibuguziwe na watafutiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema maeneo ya wafanyabiashara hayo tayari yameshatengwa huku yakiwa na mazingira ya kuweza kufanya biashara.
meenza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.
Mjema ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kuzungukia masoko ambayo wanatarajia kuwahamishia wafanyabiashara walio katika Manispaa ya Ilala, ikiwemo soko la Kivule na Kerezange ambapo kwa sasa yapo tayari huku akiahidi kushughulikiwa kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi.
Mjema amesema katika kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ni pamoja kuwa kituo cha Daladala ambapo abiria wanashuka na kupata mahitaji yao katika masoko.
Amesema soko la Tabata Muslim liko katika hatua za mwisho mpaka mwezi wa 12 masoko yote yatakuwa katika mazingira rafiki ya kufanya wafanyabiashara ndogodogo waweze kufanya biashara zao.
Mjema amesema kutokana na kuondoka kwa wafanyabiashara hao kutakuwepo wa eneo moja la barabara ambazo wafanyabiashara wataruhusiwa kufanya biashara kando kando ya barabara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi pamoja na Jumapili kuanzia majira saa sita mchana kwa wafanyabiashara
Mitaa ya Lumumba na Mkunguni itatumika kufanya biashara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili eneo hilo linauwezo wa kukaa zaidi ya wafanyabiashara 1800.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesimamia uadikishwaji wa machinga waliokuwa wafanyabiashara kandokando ya barabara za mabasi yaendayo kasi na kuwataka ambao hawajajiandikisha wajiandikishe mapema ili wapatiwe maeneo rasmi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na Wafanyabiashara ndogondogo juu ya kuwatafutia maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa mazingira rafiki kwa kufanya biashara zao , leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara ndogondogo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara Ndogondogo wakijiandikisha majini yao ili wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, leo jijini Dar es Salam.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea masoko ambayo wafanyabiashara ndogondogo watapelekwa kufanya biashara leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo ‘Machinga’ katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
No comments:
Post a Comment