HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2016

Waziri Simbachawene aagiza fedha za TASAF zirejeshwe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.

Mhe. Simbachawene pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwasimamisha kazi Waratibu wote wa TASAF wilaya ili kufanya uchunguzi wa jinsi walivyojihusisha katika kuvuruga utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kwa kuandikisha kaya zisizokuwa na sifa na ametaka wale wote watakaobainika kuhusika katika kutenda makosa mamlaka za kinidhamu kuchukua hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mhe. Simbachawene amesema usimamizi dhaifu wa mpango wa TASAF katika ngazi za halmashauri hususani Waratibu wa Mpango wa TASAF Wilaya wasiokuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yao imesababisha fedha za Mpango wa TASAF kutumiwa na watu wasiokuwa walengwa.

Waziri Simbachawene pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia hatua watumishi wa ngazi za Kata, Mitaa na Vijiji ambao kwa namna moja au nyingine watabainika kuhusika katika kuvuruga Mpango wa kuzinusuru kaya maskini kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, Mhe. Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa kujiridhisha katika mikoa yao ikiwa Wakurugenzi watachukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wasiokuwa waaminifu na kuwataka kumpelekea taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne kuanzia leo tarehe 25/11/2016.

Mheshimiwa Simbachawene ameitaja mikoa inayoongoza kwa matumizi mabaya ya fedha za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kuwa ni Dar es Salaam, Kilimanjaro, Morogoro, , Shinyanga, Arusha, Kigoma, Dodoma, Arusha na Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad