Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge
mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP)
kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.
Kiwanda hicho kinachotengeneza mabomba ya maji,
ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi
ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.
“Nimeridhishwa
na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha
mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.
“Hii
ni hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni
hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.
Inj.
Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya
Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka
nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu
muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.
Naye
Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes
Limited (TSP) alisema
nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na
kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za
wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.
Alisisitiza
bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa
kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi ikiwemo
Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.
Dhumuni
la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa
uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment