HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 6, 2016

WAMACHINGA SASA KUTUMIA ENEO LA BARABARA YA LUMUMBA JIJINI DAR KUPANGA BIASHARA ZAO

Kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli kuwataka viongozi kuwatafutia maeno ya kufanyia biashara Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga na ikiwezekana wapewe fursa ya kuzitumia baadhi ya barabara kwa shughuli hizo, Hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameanza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo, kuwaruhusu wafanyabiashara hao kutumia eneo la Barabara ya Lumumba kuweka biashara zao kwa siku tatu za wiki ambazo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Akiwa Katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya huyo amewapongeza baadhi ya machinga waliojitokeza eneo hilo na kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa hiyo yenye tija kwao.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akitembelea barabara ya Lumumba ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga kwa ajili ya machinga kufanya biashara zao kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. ambapo amewapongeza baadhi ya machinga waliojitokeza eneo hilo na kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa hiyo yenye tija kwao. Leo jijini Dar es Salaam.akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Msongela Palela, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni. na Katibu Tawala wa Wilala ya Ilala Edward Mpogolo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) wakijiandishi majini yao ili wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, leo jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) waliojitokeza katika eneo hilo wakiendelea na kazi.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika barabara ya Lumumba wakijipatia mahitaji yao ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga kwa ajili ya machinga kufanya biashara zao.

Muonekano wa barabara ya Lumumba.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad