HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2016

WAAMUZI YANGA VS SIMBA, MBEYA CITY VS YANGA WAWEKWA KIPORO

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) umeendelea kuwaweka kiporo waamuzi wa mchezo baina ya Yanga na Simba uliochezwa Oktoba 01 mwaka huu ambao ulichezeshwa na mwamuzi Martin Saanya pamoja na mwamuzi msaidizi namba moja Samuel Mpenzu.


Mwamuzi wa mchezo wa Mbeya City dhidi ya Yanga Rajab Mrope, Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi ya Coastal Union Vs KMC nao uchunguzi wao unaendelea kukamilika huku hatua ya mwisho ya uchunguzi huo ni wao kufika mbele ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ambapo watahojiwa ili kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika taarifa zao.


Katika mchezo wa Yanga na Simba, Saanya alishindwa kuhimili mchezo huo na kupelekea mashabiki wa klabu ya Simba kufanya vurugu baada ya kukubali goli lililofungwa na Mrundi Amisi Tambwe na kisha wachezaji wa timu ya Simba kumzonga na kumpa kadi nyekundu Jonas Mkude ambayo baadae kamati ya masaa 72 iliweza kuifuta na kumruhusu kuendelea kucheza mechi za ligi kuu.

Mpenzu ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi wa mchezo huo, alionyesha udhaifu kwa kukataa goli halali la Ibrahim Ajib kuwa kuonyesha kuwa ameotea.

Katika mechi ya Mbeya City dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, mwamuzi Rajab Mrope naye amepewa muda wa kujieleza mbele ya kamati ya masaa 72 baada ya kuonyesha madhaifu kwenye mchezo huo kwa kutoa maamuzi tofauti mara tatu baada ya goli la pili lililofungwa na timu ya Mbeya City kuwa na utata na timu ya Yanga kulalamika.

Naye Kamishna wa mechi ya Tanzania Prisons na Simba Jimmy Lengwe kutoka Morogoro amepewa onyo kali kwa kutoripoti baadhi ya matukio ya wazi yaliyotokea kabla ya mechi hiyo kuanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad