HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 29, 2016

TIMU YA BEACH SOCCER SASA KUIVAA UGANDA DESEMBA 09

 
 
 
 
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer)

KOCHA  Mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), John Mwansasu ameita kikosi cha wachezaji 12 kati ya 13 wanaotarajiwa kuivaa Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Desemba 9, 2016 utakaofanyika Dar es Salaam.

Mwansasu ambaye hivi karibuni kikosi chake kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio ni makipa ambao ni Rajab Galla na Khalifa Mgaya.

Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.

Kocha John Mwansasu bado anafuatilia viwango vya wachezaji mbalimbali ili kujaza nafasi moja ya kipa kabla ya Desemba mosi, 2016 baada ya Kipa Juma Kaseja kutoa taarifa kuwa atakuwa na udhuru wakati nyota mwingine, Mohammed Banka aliyeripotiwa kuwa safarini nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad