HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2016

THAMINI UHAI YAKABIDHI PIKIPIKI ZENYE THAMANI YA SHILINGI 40 MIL KWA MGANGA MKUU MKOA WA KIGOMA

 Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Thamni Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji na utekelezaji wa shughuli za shirika wakati wa Hafla ya kukabidhi pikipiki 9 zenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma ambapo zitatumika kwenye vituo vya afya mkoani Kigoma.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (Wa Tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi kwa serikali ya mkoa Kigoma pikipiki 9 zenye thamani ya shilingi milioni 40 ambazo zitatumika kwenye vituo vya afya mkoani humo.
Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Paul Chaote (kati kati aliyesimama)  akitoa hotuba kwa niaba ya Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Charles Palangyo wakati wa Hafla ya shirika la Thamini Uhai kukabidhi kwa serikali ya mkoa Kigoma jumla ya pikipiki tisa zenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya matumzi kwenye vituo vya afya mkoani Kigoma,
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (kulia) akikabidhi moja ya pikipiki tisa zenye thamani ya shilingi milioni 40 Kwa Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Dk.Paul Chaote  kwa niaba ya Katibu tawala wa mkoa Kigoma Charles Palangyo ambao pikipiki hizo zitatumika kwenye vituo vya afya mkoani humo.


Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Paul Chaote (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa Vitus Bukombe  Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Ilagala (kati kati) ikiwa ni moja ya pikipiki tisa zilizotolewa na shirika la Thamini Uhai kwa vituo vya afya mkoani Kigoma kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kukabiliana na vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Thaimini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (wa pili kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya pikipi tisa zenye thamani ya shilingi milioni 40 zilizotlewa na shirika hilo kwa serikali ya mkoa Kigoma (wa pili kushoto mstari wa mbele) Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk.Paul Chaote.
(Picha Zote na Fadhili Abdallah)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad