HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 8, 2016

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA ELIMU KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TATU, MH. JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA

 Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya awamu ya tatu  Mhe. Joseph Mungai (pichani), amefariki dunia leo majira ya saa 11 jioni. 

Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)
"Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki, tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili siyo sahihi" Amesema Eligaesha.


Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia, na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike, kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili. Habari kamili ya msiba huo zitawajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia. Mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.  
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.  Mungu ilaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad