HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 7, 2016

TANZIA: MZEE SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MATIBABU UJERUMANI

Taarifa zilizotufikia mapema alfajiri zinasema kuwa aliyekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mhe. Samuel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Ujerumani akiwa katika matibabu, mtoto wa marehemu Bw. Benjamin Sitta, amethibitisha.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi kwa kadri zitavyopatikana.
Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi
- Amin

***********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta.

Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.


“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.


“Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.


Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni”

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Novemba, 2016
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad