HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2016

TANZANIA YAZIDI KUPOTEA, YASHUKA MPAKA NAFASI YA 160


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TANZANIA yaendelea kusuasua katika soka na kushuka kwa nafasi 16 na kufikia nafasi ya 160  na 48 kwa Afrika huku Argentina wakiendelea kushika namba moja kidunia.


Viwango hivyo vya FIFA vimekuja baada ya michezo ya kirafiki iliyofanyika kuanzia  Novemba 13-17 na Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki na Zimbabwe na kuambulia kufungwa goli 3-0.

Chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa timu ya Taifa imekuwa haina mafanikio kwa kushindwa kupanda au kupata matokeo mazuri kwa kucheza mechi 11, kushinda 1 kutoka sare tatu na kufungwa mechi saba.

Argentina licha ya kufungwa wameendelea kushika namba moja kidunia, Senegal wameshika nafasi ya 33 kidunia na namba moja kwa Afrika ikifuatiwa na Ivory Coast nafasi ya 34,Tunisia  35, Misri 35 na Algeria wakishika nafasi ya 38.

 Nchi za Afrika zimeonekana kushindwa kufurukuta mbele dhidi ya matafifa ya Ulaya na America hasa baada ya kushindwa kuingiza timu kwenye timu 20 bora.

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani  wameshushwa kwa nafasi moja mpaka nafasi ya tatu na Brazili kukaa nafasi ya pili.

Viwango vingine vya Fifa vitatolewa tena  Desemba 22, 2016 - ambayo itatoa timu ya mwaka  na mwanzilishi wa Mwaka.


msaada kutoka FIFA.COM RANKING





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad