HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 29, 2016

SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA SEKTA YA HABARI

 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wajumbe wa Serikali ya China (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana  Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wa Serikali ya China wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali  imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya China katika kuimarisha sekta ya habari  ili kuendana  na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya utoaji wa habari.
Hayo  yamesemwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  jana Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo  na Naibu  Waziri wa Uenezi  wa China Ndg. Sun Zhijun yaliyolenga kuimarisha sekta ya habari nchini.
“Tunashukuru kwa uhusiano mzuri uliopo baina ya serikali zetu  ikiwemo hii ya  kuendeleza sekta ya habari ambayo ni muhimu  na inamchango mkubwa katika kuleta maendeleo na kutoa ajira kwa watanzania”.Alisema Mhe Nape.
Mhe. Nape anaongeza kuwa ushirikiano huo  utasaidia nchi zote mbili kuwa na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi kupitia vipindi mbalimbali vinatakavyokuwa vikirushwa na vyombo vya habari vya nchi hizo kwa lugha zote mbili.
Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri wa Uenezi wa China Mhe.Sun Zhijun ameahidi kufanya mageuzi katika soko la habari kupitia radio na Luninga ambazo  zitatoa fursa ya kuonyesha vipindi mbalimbali vya Kiswahili na hivyo kusaidia katika kukuza na kueneza lugha hiyo.
“Ushirikiano wetu ni wa tangu enzi na enzi hivyo ni budi kuutunza na kuulinda umoja wetu ndo maana tukaona kuna umuhimu  wa kuimarisha  sekta ya habari ambapo Serikali yetu ya China itakuwa ikirusha  vipindi vya radio na luninga kama vile muziki na filamu za kiswahili katika vyombo vyetu vya habari ”.Alisema Mhe.Zhijun.

Vyombo vya Habari vya Tanzania na China vimekuwa vikishirikiana katika kubadilishana Habari na vipindi mbalimbali kupitia Chaneli zao na hivyo kusaidia ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kuendelea  kuimarika na kustawi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad