HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 17, 2016

MREMBO JULITHA KABETE AAHIDI MAKUBWA MISS AFRIKA

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika, Julitha Kabete ameondoka leo kuelekea nchini Nigeria katika fainali ya michuano hiyo inayofanyika Novemba 26 mwaka huu huku akiwaahidi watanzania kwua  ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania .

Akizungumza kabla ya kuondoka kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kabete amesema kuwa lengo lake ni kuwa mmoja wa wawakilishi bora katika shindano hilo na kuitangaza vyema nchini  pamoja na kurudi taji hilo na kwa kupitia kampuni ya Millen Magese Group chini ya Mkurugenzi wake ,Happiness 'Millen' Magese ameshukuru kwa kuingia nae mkataba ili aweze kushiriki michuano hiyo na kufanya Kazi nyingine za urembo. 

"Mimi kama mwakilishi wa Tanzania nitahalikisha anafanya vizuri katika shindano hilo, ambalo nimepata nafasi ya kuwa mpeperusha bendera wa nchini yangu Tanzania " amesema. Kabete alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ambaye alimshihi kwenda kujituma zaidi kwani wana imani na uwezo wake na pia ni moja ya warembo watakaowakilisha vyema nchi yetu na kurudi na taji hilo.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa nyingine si tu akishapatikana mshinda wengine wanaachwa, hivyo tunaamini mrembo huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri,” amesema Nape.

Shindano hilo litafanyika nchini humo katika jimbo la Cross River, mji wa Calabar,ambapo Gavana wa jimbo hilo la Cross River Profesa Ben Ayade, atatoa zawadi ya gari na zaidi ya sh.million 52 ya Tanzania hiyo itakuwa kwa ushindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata zawadi ya Sh.milioni 32 na ushindi wa Tatu ni Sh.million 22. 

Shindano hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli
mbiu ya Kutunza, Kujali na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili ya Maendeleo endelevu.
Julietha alichaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG), inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo pamoja na 
Mmratibu wa MMG, Matukio Chuma, amesema kuwa wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week.

Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani na nje ya Bara la Afrika. mwisho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad