HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2016

MIGOGORO YA NDOA, ARDHI NA MATUNZO YA WATOTO YAONGOZA KUSUMBUA WANANCHI

 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari akiwataarifu kuhusu kusomwa Bungeni kwa mara ya kwanza kwa Muswada wa Sheria ya Msaada wa Kisheria wenye lengo la kuwa sheria yitakayosimamia na kuratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili.
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria  Bi .Felistas Mushi akiongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari kuhusu namna sheria ya Msaada wa Kisheria itakapopitishwa namna itakavyofanya kazi na kuwasimamia watoa huduma za msaada wa kisheria.
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha moja ya majarida yaliyotayarishwa na Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria katika kuelimisha Umma wakati Mratibu wa Sekretarieti hiyo Bw. Daniel Lema (kushoto) akielezea juu ya upatikanaji wa msaada wa kisheria hasa kupitia wasaidizi wa kisheria (paralegals). Mwingine pichani ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria  Bi .Felistas Mushi.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo leo (23/11/2016) katika ukumbi wa Mikutano Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad