HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 7, 2016

MANISPAA YA ILALA KUIBURUZA POLISI KAMPUNI YA TAMBAZA.

Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeamua kuishtaki kampuni ya udalali ya TAMBAZA kwa jeshi la Polisi kutokaana na kuingilia mamlaka ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Wilaya Ilala.


Hayo yamesemwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo ,Omar Kumbilamoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao ni wawekezaji kutoka nchi mbalimbali.

"Kampuni hii imetutia hasara ya kuweza kupungua kwa mapato kutoka million tatu hadi milioni moja kwa siku jambo ambalo linaturudisha nyuma katika kusukuma gurudumu la maendeleo kutokana na mzigo mkubwa tulionao wa kuhudumia wananchi"amesema Kumbilamoto.

Amesema wawekezaji kwa sasa wamekuwa hawana amani kutokana na hali halisi inayofanywa na kampuni hiyo kuwazuia wasipakue mizigo yao na kuwataka walipe tena licha ya kuwaonesha risiti ya malipo kutoka kwa halmashauri.

Ameongeza kuwa,Halmashauri ndio yenye dhamana ya kuweza kuwashugulikia changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi pamoja na kuwatatulia kero mbalimbali ikiwemo kukarabati barabara,kuzoa taka,kutoa huduma nzuri Hospitalini,kulipa walimu na sio kutoka halmashauri ya Jiji.

Kwa upande wake Ofisa Afya wa manispaa hiyo kitengo cha usafirishaji Cosmas Mwatete amesema,ni jambo la kusikitisha sana kitendo kinachofanywa na kampuni hiyo kwani wanavuruga mwaliko wa Rais kutoka kwa wawekezaji ambao wanaingia nchini.

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kampuni ya Tambaza kukamata kontena zinazoingia manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam , Kushoto ni Afisa Msaidizi wa Masoko Manispaa ya Ilala, Cosmas Mwaitete
Afisa Msaidizi wa Masoko Manispaa ya Ilala, Cosmas Mwaitete akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kampuni ya Tambaza kukamata kontena zinazoingia manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad