Friday, November 25, 2016

MAKONDA AMUAGIZA MEYA MTEULE WA MANISPAA YA UBUNGO KUHAKIKISHA ANAMALIZA CHANGAMOTO YA MADARASA MATANO KATIKA SHULE YA SEKONDARI URAFIKI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuagiza Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni Meya Mteule wa Manispaa hiyo Boniphace Jacob kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano katika shule  ya Sekondari Urafiki.
RC Makonda ameyasema hayo wakati anazindua shule hiyo ya urafiki ikiwa ni moja ya muendelezo wa ziara ya siku 10 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
RC Makonda amesema viongozi wa kisiasa inabidi waache siasa za ujanja ujanja na badala yake kuwatumikia wananchi
"Diwani wa hapa anatakribani miaka mitano hivyo inabidi apambane na kuhakikisha uhaba wa vyumba hivyo vitano unakamilika"
katika hatua nyingine RC Makonda amewataka wanafunzi kujitahidi kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuingia katika soko la ushindani wa ajira kwa vitu vingi vimetawaliwa na Sayansi.
Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea pia barabara ya Ubungo River Side na kuwataka wananchi wajitolee maeneo yao ili kupisha ujenzi wa barabara ambao ulikuwa ni changamoto kwao
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akikata uteoe wakati wa uzindua shule ya Sekondari Urafiki leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka jiwe la Msingi katika shule ya Sekondari Urafiki leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akigangua viwanda  vya Paper Kraft kilichopo na cha Tanzania Tooku vilivyopo Mabibo Extenal leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akikagua ujenzi wa barabara ya ilipo katika Mtaa wa Kibangu  Kata ya  Makubuli unaoanzia Riverside mpaka kwa Mzee wa Upako ambapo pia alisikiliza kero za wananchi  walio pisha upanuaji wa Barabara leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda. alisikiliza kero za wananchi  waliopisha upanuaji wa Barabara ilipo katika Mtaa wa Kibangu  Kata ya  Makubuli leo jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment