Balozi Hemed Mgaza kushoto alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Dkt Mohamed Ali Shein akiwa nchini Tanzania. Picha na Maktaba.
Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia
JOPO la Madaktari Bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wanatarajiwa kuwasili Zanzibar Novemba 11 kwa ajili ya kuweka kambi ya kutoa matibabu (Medical Camp) katika Hospitali za Chake Chake na Wete kwenye Kisiwa cha Pemba.
Programu hii inaratibiwa
na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu ya Saudi Arabia World Assembly
of Muslim Youth – WAMY kwa ajili ya kwenda nchini Tanzania katika kisiwa cha
Pemba kutoka huduma hiyo ya afya.
Akizungumza mjini hapa,
Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Hemed Mgaza, alisema kwamba msafara wa
madaktari hao utakuwa na tija kwa Watanzania wote, hususan wa Kiwa cha Pemba.
Alisema kwamba taratibu
zote za madaktari hao zimekamilika, huku ratiba yao ikionekana kwamba
watahudumia kuanzia Novemba 11 hadi 22 kabla ya kuekea na ratiba zao ambapo
ni jambo la kujivunia kwa wataalam hao kuamua kwenda nyumbani Tanzania kutumia
taaluma zao.
“Madaktari hao watatoa
huduma ya matibabu kwa muda wa siku kumi bila malipo kuanzia tarehe 11 hadi 22
mwezi Novemba, 2016 kama taarifa za msafara wao zinavyoonekana katika ofisi
zetu.
“Pamoja na kutoa huduma
za matibabu, Madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali
ambavyo mwisho wa kambi hiyo watavitoa msaada kwenye hospitali hizo,” alisema.
Kwa mujibu wa Balozi
Mgaza, ujio wa madaktari hao ni wa mara ya kwanza nchini Tanzania na
wanatarajia kutoa huduma hizo sehemu nyingine za Tanzania siku zijazo baada ya
kukamilisha awamu ya kwanza, huku madaktari hao wakiwa wameshatoa huduma kama
hizo katika nchi za Comoro, Cameroon na kwingineko.
No comments:
Post a Comment