HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 3, 2016

KINDA MTANZANIA ANAYEKIPIGA KENYA ATAMANI LIGI YA NYUMBANI


MSHAMBULIAJI kinda mwenye asili ya kitanzania anayekipiga nchini Kenya ameweka wazi msimamo wake wa kutamani kucheza ligi ya Tanzania hasa baada ya mkataba wake kumalizika na timu ya Agro Chemical iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la Kwanza ijulikanayo kama National Super League.


Akizungumza na mtandao wa Michuzi  Globu, kinda huyo kutoka zao la Copa Coca Cola Jerome Nturukindo amesema kuwa mkataba wake umeisha na anachokitamani kwa sasa ni kuja kucheza ligi ya nyumbani kwani anajua ni moja ya ligi yenye ushindani sana Afrika Mashariki na Kati.

Nturukindo amesema kuwa, toka alivyoondoka nchini mwaka 2013 akitokea timu ya vijana ya chini ya miaka 20 African Lyon ambapo walimchukua kutoka mashindano ya Copa Colachini ya miaka 17 kutoka timu ya Temeke na tayari amechezea timu ya St Joseph na Agro Chemical za nchini humo.

Kutokana na mapenzi yake makubwa ya mpira na kutaka kuisaidia timu yake katika Nturukindo amesema kuwa kwa sasa anarejea nchini rasmi na yupo tayari kufanya mazungumzo na timu yoyote itakayohitaji huduma yake kwani yeye mpira ndio kazi.

Mwaka jana alifanikiwa kwenda kwenye majaribio nchini Serbia na alifanya vizuri na wakamuahidi kuwa katika dirisha dogo la mwezi Januari watamuita ila akaona kimya na hawakumpa taarifa yoyote mpaka mda huu.

Katika msimu wa 2015/2016 Nturukindo ameweza kuifungia timu yake goli 16 kati ya mechi 25 na ligi inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Novemba na itakapomalizika tu anarejea Tanzania kuja kutafuta timu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad