HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 30, 2016

FEDHA ZINAZOKUSANYWA NA SERIKALI ZINAKWENDA KATIKA MIRADI –MSAJILI WA HAZINA


Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya mzunguko wa fedha leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema mzunguko wa fedha sio mzuri kutokana na fedha nyingi  kwenda katika  miradi ya  kuimarisha huduma kwa wananchi.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru wakati akizungumza na waandishi habari juu ya taarifa zinazosambaa  zinazodai kuwa benki zimeyumba.
Amesema serikali katika kudhibiti fedha za umma katika mashirika na taasisi ni kuwa na akaunti benki kuu ili kuweza fedha hizo kuonekana na sio kuwa katika benki zingine.
Mafuru amesema kuyumba kwa taasisi za fedha  haitokani na kuondolewa kwa kiasi cha sh.bilioni 515 kwa kila taasisi kuwa na akaunti benki kuu.
Amesema taasisi za fedha kwa septemba zimekopesha sh.trioni 16 kati ya fedha hizo sh.trioni 1.4 ni mikopo mibovu hivyo kwa benki lazima ziyumbe kwa muda kutokana na mikopo hiyo mibovu.
Mafuru amesema kupanga ni kuchagua hivyo serikali imetaka kuimarisha huduma kwa wananchi , lazima kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika huduma za kijamii.
Amesema viwanda vikijengwa hapa  nchini wananchi watanunua bidhaa za ndani hivyo fedha itazunguka hapa hapa kuliko kununua bidhaa za nje ambazo fedha zinakwenda kuwapa maendeleo  nchi nyingine.
  
Aidha amesema kuwa nia Rais Dk. John Pombe Magufuli ni njema ya kutaka kuimarisha huduma kwa wananchi katika miradi mbalimbali zinazokusanywa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad