HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 15, 2016

DIRISHA LA USAJILI LIGI KUU LAFUNGULIWA RASMI LEO


Ofisa wa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
DIRISHA la usajili wa ligi kuu limezinduliwa rasmi leo ambapo linatarajiwa kufungwa Desemba 15 mwaka huu hku timu zikishauriwa kufanya usajili kwa umakini kwa ajili ya kupata wachezaji wazuri watakaosaidia timu zao kuleta ushindani kwenye ligi kuu raundi ya pili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa wa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa kufunguliwa kwa dirisha hili la usajili linawapa nafasi vilabu kuhakikisha wanafanya usajili kwa umakini ili kuweza kuepukana na migongano baina ya timu na timu na litadumu kwa mwezi mmoja kuanzia leo Novemba 15 mpaka Desemba 15 kabla ya ligi kuanza raundi ya pili.

Lucas amesema kuwa raundi ya pili inatarajiwa kuanza Desemba 17 ila bado utaratibu wa ratiba haujamalizika ila tunatarajia kuwa mapema hivi karibuni tutatoa na kuiweka wazi kila mmoja ajue anaanzia wapi na anamaliza na nani.

Mbali na hilo amesema timu za taifa za Twiga Stars na Taifa Stars zimewasili jana usiku majira ya saa 3 na tayari makocha wote wameshavunja kambi na wachezaji wameenda mapumziko wakisubiri kuungana  na timu zao kwa ajili ya kuanza duru la pili kwa ligi kuu Vodacom na ligi ya wanawake.

Taifa Stars iliweza kufungwa kwa goli 3-0 na timu ya taifa ya Zimbabwe huku Twiga Stars wakiweza kujibu mapigo kwa Cameroon kwa kuwafunga 2-1 baada ya uke mchezo wa kwanza kufungwa 2-0 na kuwaacha midomo wazi wachezaji wa Cameroon.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad