HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 14, 2016

WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WATUA JIJINI ARUSHA, SHINDANO HILO KUFANYIKA JIJINI MWANZA OKTOBA 29

Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchi wanaowania taji la mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2016/17), wameanza rasmi ziara yao ya siku tatu mkoani Arusha ambapo watatembelea maeneo mbalimbali yaliyopo mkoani humo.


Akizumza na wanahabari, Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapo leo na wanakaa kwa muda wa siku tatu, na katika siku hizo wanampango wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Aidha alisema kuwa, pia ndani ya siku hizo tatu Warembo hao watachuana kwenye kinyang'anyiro cha 'Top model' kitakachofanyika Jumamosi Oktoba 15 katika ukumbi wa Triple A ulipo ndani ya jiji la Arusha 

"tunafanya shindano hilo katika ukumbi wa triple A na tunatarajia wananchi wengi wa Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo ni shilingi 10000 tu, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwaalika wananchi wa Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa 'Top Model' wa Miss Tanzania"alisema Makoye 

Mbali na kutembelea Mkoa huo wa Arusha, warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Singinda na Dar es Salaam na wanatarajiwa kuelekea Mkoani Mwanza ambako ndipo shindano la Miss Tanzania mwaka huu linafayanyika kwa mwaka huu .

Shindano la 'Miss Tanzania 2016' linatarajiwa kufanyika Oktoba 29 katika ukumbi wa Rock City Mall na warembo wote 30 wapo vizuri na wanasubiria siku yenyewe ifike na maandalizi yashindano yamekamila.

 

Baadhi ya Warembo wanaoshiriki kinyanganyiro cha kumsala 'Miss Tanzania' wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa ofisi za gazeti la Guardian zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha mara baada ya kutembelea.NA WOINDE SHIZZA, ARUSHA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad