HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 1, 2016

demo-image

TICTS YASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI KTI SHULE YA SEKONDARI KURASINI JIJINI DAR

 KAMPUNI ya TICTS inayojishughulisha na kazi ya uendeshaji wa huduma za bandari, Dar es salaam imeendelea na kampeni ya yake ya "Go GREEN" kwa kupanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari Mivinjeni, Wilayani Temeke.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini hapa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa alisema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2015, suala la upandaji miti ni lazima kufanyika ili kuenda sambamba mkakati huo.

"Tukiwa na miti michache au miti iliyotoweka, tutaangamia kama taifa na ikiwa tutakuwa na miti mingi, hapo hatuna cha kupoteza, ila tukiruhusu ukataji miti uendelee katika nchi yetu bila kupanda mingine, tutaishia kuwa ombaomba kama si kufa kwa njaa" alisema Talawa.

Pia alitoa wito kwa makampuni mengine yanayofanya biashara hapa nchini, kuisaidia Serikali kuhamasisha masuala yenye manufaa kwa taifa kama hilo la kupanda miti.
MMG_2755
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akishiriki kupanda Mti katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, kupitia Kampeni yao ya "Go GREEN" yenye kuhamasisha jamii umuhimu wa kupanda miti. 
MMG_2770
 Meneja wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari wa Kampuni ya TICTS, Hassan Mageta (kati) akimwagilia maji mti wake muda mfupi baada ya kuupanda katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
MMG_2787
 Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya TICTS, Caroline Owenya (kushoto) akishirikiana kupanda mti na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Mwl. Marcelino Fussi (katikati) pamoja na mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
MMG_2836
 Mwanafunzi wa Kidato ya tatu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Zahrat Mteleke akionyesha baadhi ya miche ya miti yake kabla ya kwenda kuipanda katika eneo la shule hiyo. 
MMG_2858
MMG_2874
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akikabidhi kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Mwl. Marcelino Fussi sehemu ya msaada wa vifaa vya usafi vitakavyotumiwa shuleni hapo.
MMG_2904
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kurasini na Walimu wao wakita katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la upandaji miti.
MMG_2492
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa zoezi la upandaji miti kupitia Kameni yao ya "Go GREEN".
MMG_2547
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akizungumza na washirikiwa wa zoezi la upandaji miti.MMG_2649
MMG_2581
MMG_2599
MMG_2699
Wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS wakipanda miti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *