HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 8, 2016

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi mgeni rasmi Dar Rotary Marathon 2016.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NCHI nne zinatarajiwa kushiriki mbio za Dar Rotary Marathon 2016 zitakazofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 14 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambaye atashiriki matembezi ya Km. 5.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, mbio hizo za kila mwaka huandaliwa na Dar Rotary Club kwa kushirikiana na Bank M zikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii na Mwaka huu wataelekeza nguvu zaidi kwenye ujenzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Zavalla, amesema waandaaji mwaka huu wametoa nafasi kwa nchi za Kenya, Malawi, Rwanda na Ethiopia kushiriki mbio hizo za Km 21. "Tayari sisi kama shirikisho tumetuma mialiko kupitia mashirikisho ya nchi husika na tayari wametujibu na kututumia majina ya wanariadha na makocha watakaokuja kushiriki, isipokuwa Ethiopia tu bado hawajatuma ingawa walisema watashiriki,” amesema Zavalla.

Katibu Msaidizi huyo, amesema Kenya itawakilishwa na wanariadha saba ambao ni Timothy Raibuni, Martin Musyoka, Patrick Munyithya, Willy Mwangi, Patrick Mutunga huku wanawake ni Damaris Maundu na Shelmith Muriuki wakiwa na Kocha James Mbiti.

Kwa upande wa Malawi itawakilishwa na wanariadha sita ambao ni Francis Khanje, Happy Mcherenje, Chancy Master, Rashid Taimu, Grevazio Mpani, Elija Kanyenda huku wanawake ni Cecilia Mhango na Kocha ni A. Sande na  Rwanda itawakilishwa na wanariadha wawili Eric Sabahire na Salome Nyirarukando.

Aidha, Zavalla amebainisha kuwa pia waandaaji wametoa ufadhili kwa baadhi ya wanariadha wa Tanzania ambako watagharamia usafiri na malazi, ambao ni Emmanuel Giniki, Ismail Juma,  Panga, Fabian Joseph, Dickson Marwa, Gabriel Gerald, Mshindi wa tano Marathon Olimpiki Rio 2016, Alphonce Felix huku wanawake ni Catherine Lange na Mary Naali wakiwa na Kocha Francis John na kutoka Zanzibar ni Filipo Mambo, Mohamed Mgeni, huku wanawake ni Maria Michael na Asma Mukhandi wakiwa na Kocha Hamza Haji.

Kwa upande wa zawadi, Zavalla amesema mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 3, wa pili milioni 2 na watatu milioni 1. Pia washindi wa nne hadi kumi watakuwa na zawadi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad