HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 6, 2016

OCEAN ROAD YAANDAA MATEMBEZI YA HISANI KUCHANGIA SARATANI YA MATITI.

 Afisa Mtendaji Mkuu Mkoa, Sulaiman Shahabuddin akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam akielezea namna Matembezi hayo ya hisani yalivyosaidia katika Kuhamasisha upimaji wa Saratani ya matiti nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Julius Mwaisegile akizungumza na waandishi wa habari kuelekea matembezi ya hisani yanayotarajiwa kufanyika Okotoba 28 mwaka huu. Kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu Mkoa, Sulaiman Sahahabuddin.
  Meneja Mauzo wa Hoteli ya Kunduchi Beach Winnie Kimotho akizungumza na waandishi wa habari kuelekea matembezi ya hisani ya kuhamasisha upimaji na uchangiaji wa fedha za kununulia vifaa tiba vya Chemotherapy. Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Julius Mwaisegele.

Na Zainab Nyamka, Globu ha Jamii.
TAASISI ya Saratani ya Hospital ya Ocean Road imeandaa matembezi ya hisani kwa lengo la Kuhamasisha na kuchangia zaidi ya milioni 120 zinazohitajika kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya chemotherapy.

Matembezi hayo yanayitarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, yataanzia Hospitali ya Ocean road na kumalizika hapo hapo na yataongozwa na Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis Kigwangala.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Julius Mwaiselage amesema kuwa huu ni mwaka wa nne toka kuanza kufanya matembezi ya hisani na kuchangia na pia itakuwa na lengo la kuhamasisha upimaji wa saratani ya matiti.

Mwaisegele amesema kuwa mbali na kuhamasisha upimaji huo, pia wananchi watapima bure saratani ya matiti na saratani ya shingo ya kizazi  ambapo kila mwaka watu 44,000 wanagundulika wakiwa tayari wako katika Maambukizi ya kiwango cha juu.

Mwaisegele ametoa ushauri kuwa mpaka ifikapo mwaka 2030 takribani watu milioni 22 watakuwa wana saratani ambapo kwa sasa milioni 14 wanakuwa tayari wana saratani na milioni 8.2 wanafariki kwa ugonjwa huo duniani.

Matembezi hayo yatakuwa kwa ushirikiano na Hotel ya Kunduchi Beach na Meneja Masoko wa Hoteli hiyo Winnie Kimotho amesema kuwa wanafurahi kushirikiana na Ocean Road kwa kipindi chote na wataendelea kufanya hivyo kwani wanahitaji kuona saratani inakwisha kabisa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad