HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 29, 2016

MKURUGENZI IDARA YA MAAFA APOKEA MIFUKO 640 YA SARUJI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAAFA KAGERA.

Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza) akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta wakati wa uhakiki wa misaada ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera tarehe 28 Oktoba, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akieleza jambo wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya Kamal ili kupokea na kuangalia saruji zilizokabidhiwa na ofisi hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta (wa kwanza kulia) akizungumza jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walipofika katika ofisi hizo kuangalia msaada wa safuji mifuko 640 unaosafirishwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. 
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya akiwa na Meneja Rasilimaliwatu wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Bw. Ajay Jha wakati wa kuangalia saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera Oktoba 28, 2016. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya mara baada ya kuangalia msaada wa saruji mifuko 640 uliotolewa na kampuni hiyo tayari kwa kusafirisha mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad