HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 21, 2016

MANJI AWATAKA WANACHAMA KUJITOKEZA KWA WINGI JUMAPILI HII KWENYE MKUTANO MKUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano mkuu wa dharula  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 23, Jumapili kwenye  Uwanja wa Kaunda Makao makuu ya Jangwani.

Akizungumza na wanahabari, Manji amesema kuwa wanachama wote wajitokeze siku hiyo kwani katika njia mojawapo ya kuijenga Yanga Imara ni wanachama kuchangia katika suala la maendeleo ikiwemo mabadiliko yanayotarajiwa kujitokeza ya kwenda kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa kutoka mikononi mwa wanachama na kwenda kampuni ya Yanga Yetu.
Mkutano huo wa dharula wenye ajenda 13, ikiwemo ya mabadiliko ya uendeshaji  pamoja na hatma ya Mwenyekiti wa klabu hiyo kuendelea na nafasi yake au kujiuzulu umekuwa ukizungumziwa sana katika vyombo vya habari na baadhi ya wanachama kupinga mabadiliko hayo na hata kutaka ajiuzulu nyadhifa yake.

Manji amesema kuwa, kuja kwa wingi kwa wanachama kutasaidia kujadiliana kwa hoja na kupata mapendekezo yao na kulingana na katiba ya Yanga mwanachama ambaye hajalipia ada yake kwa kipindi cha miezi sita anakuwa ameshajifuta uanachama na atatakiwa aende kuomba katika tawi lake.

Akiongelea suala la Uwanja wa mazoezi, Manji amesema kuwa katika makubaliano ya mkataba wao ujenzi wa Uwanja huo utaanza kujengwa ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni.

Aidha Manji amesema kuhusu suala la kusainiwa kwa mkataba na bodi ya wadhamini dhidi ya kampuni ya Yanga Yetu kila kitu kitajadiliwa kwenye mkutano huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad