HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2016

MAFUNZO MAALUM KWA MATUMIZI YA VIFAA VYA KUIMARISHA HUDUMA KWA WATOTO WACHANGA YATOLEWA NA CCBRT.

 Dr. Mchomvu kutoka CCBRT  akitoa mafunzo kwa Madaktari walioshiriki katika mafunzo ya kutumia Vifaa hivyo ili kufanya  zoezi hilo kwa ufanisi liweze kuleta matokeo mazuri.
 Muuguzi msaidizi  wa watoto katika hospitali ya Muhimbili Bi. Miriam ambaye pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaonufaika na mafunzo hayo akifurahi jambo wakati wa mafunzo hayo yakiendelea.Bi Miriam alisema mafunzo hayo yatawaongezea ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi.
Mkufunzi Mkuu wa mafunzo hayo Daktari,Yaser Abdallah amesisitiza umuhima wa elimu Zaidi kutolewa kwa wauguzi na kusisitiza kwamba mafunzo hayo yatolewe kwa kiwango cha juu Zaidi Anaiomba serikali ya Tanzani pamoka na wadau wengine  kuunga mkono kujitahidi zinazofanywa na CCBRT kutoa misaada Zaidi na kushiriki kwa pamoja kuboresha huduma ya afya katika hospitali zote na sio tu hospital za rufaa.

KUPITIA Mpango wa kutoa mafunzo ya Uzazi na vichanga (Maternal & Newborn) unaofanya kazi kwa wasaidizi wa Afya kutoka kwenye vituo 23 katika mkoa wa Dar Es Salaam.

 CCBRT kwa kuendeleza jitihada zake za kuhakikisha inapunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wanaozaliwa kabla ya muda imeanza rasmi    kutoa mafunzo maalum ya jinsi ya kutumia  vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya  kuwasaidia kuboresha huduma kwa watoto wachanga.

 Mpango huu umewezeshwa na Vodacom Foundation na mafunzo haya  maalum yatasaidia  wauguzi ili kuweza kuvitumia Vifaa hivyo kwa ufanisi Zaidi katika jitihada za kupunguza  vifo vya watoto wachanga,watoto wanaozaliwa kabla ya muda (pre maturity), watoto wanaozaliwa na maambukizi na wale wanaozaliwa  na tatizo la mfumo wa hewa. Lengo kuu ni kushiriki katika harakati za kupunguza vifo vya watoto wachanga katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Wataalam wa kiufundi waliotengeneza vifaa hivyo  nao wamefika nchini  kutoa mafunzo kwa madaktari wa watoto wachanga kuhusu jinsi ya kuvitumia na kuvitunza vifaa hivyo, pia kwa makampuni ya Kitanzania kwa ajili ya urekebishaji kama vikipata hitilafu. 

Mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa muda wa wiki moja katika hospital kuu  ya Rufaa  Muhimbili yamejumuisha wauguzi wa watoto wachanga kutoka hospital kuu za rufaa mkoani Dar es salaam ambazo ni Temeke Amana ,Mbagala na Mwananyamala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad