HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 8, 2016

KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU CHA DOGODOGO MALTIPORPUSE TRAINING CENTRE BUNJU CHA PATA MSAADA KUTOKA TAASISI YA MATHAYO SULEIMAN.

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Mathayo Suleiman Foundation yatoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman, amesema kidogo walicho nacho kinaweza kuwasogeza siku mbili tatu watoto wanaoishi katika kituo hicho kwani kinakabiliwa na uhaba wa chakula kwa kiasi kikubwa sana.

Pia amesema kuwa katika maisha tumetofautiana ndio maana wanachama wa taasisi hiyo wameona watoe kile kidogo walichokuwa nacho kwani kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Nae Mratibu wa Kituo  cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera amewashukuru wanachama wa Taasisi hiyo kwa kutoa mchango wao kwani taasisi ilikuwa katika hali mbaya sana ya ukosefu wa chakula.

Amesema kuwa kituo hicho  Dogodogo Maltiporpuse Training Centre  mpaka sasa kinawatoto 39 wasichana 10 na wavulana 29 amesema kituo hicho Kilifunguliwa 2003 kwa lengo la kuwapika kiufundi watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kujitegemea wakiwa na nyenzo mhimu ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa uhaba wa chakula ukiendelea kituo hicho kitafungwa kwani mpaka sasa wanahitaji zaidi ya Milioni 205 kwaajili ya chakula pamoja na vifaa vya kuwapa kila mhitimu wa mafunzo yanayotolewa katika kituo hicho.
 Mratibu wa Taasisi ya Mathayo Suleiman, Banga Suleiman(Mwenye Suluali Nyeupe) akishirikiana na wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation wakikabidhi unga kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman (Mwenye suti nyeusi katikati) akikabidhi mbuzi kwaajili ya nyama kwa Mwalimu wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Rosemary Nyabuzuki leo. Wengine ni wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman.



  Baadhi ya wanachama wa taasisi ya Mathayo suleiman wakikabidhi msaada kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Kituo  cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera akiwashukuru wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman kwa jinsi walivyojitoa katika kuchangia kituo hicho msaada wa chakula pamoja na vitu mbalimbali.
  Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo mara baada ya wanachama hao kutembelea katika kituo hicho na kujionea baadhi ya Shughuli zinazofaywa na watoto hao katika kituo hicho.

 Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera katika kituo hicho leo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman akizungumza mara baada ya kupata maelezo ya kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kituo cha 

Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman wakiangalia meza ya kukunja na kukunjua walipotemelea katika Darasa la uchongaji Vitu vya Samani walipotembelea katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salam leo.
Baadhi ya Samani zilizochongwa na watoto wa kituo chA Dogodogo Multiporpuse Training Centre.


 Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman wakipata maelezo walipotembelea katika darasa la ushonaji nguo kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Bunju jijini Dar es Salaam leo. 
 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman akiwa na wanachama wa taasisi hiyo wakiangalia ngoma inayochezwa na watoto wa kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo.


  Wanachama wa  Taasisi ya Mathayo Suleiman wakitembelea mabweni ya watoto hao.

 Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre wakifanya mazoezi ya kuzima moto endapo kukitokea tatizo la nymba kuungua.
 Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre wakiwa katika picha ya pamoja.

 Wafanyakazi wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo.


 Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo wakimuokoa mtu aliye juu ya ghorofa wakati wa tatizo la Moto.
 Mtu aliyekuwa juu ya Ghorofa mara baada ya kupata msaada wa kutolewa eneo la Tatizo la Moto.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad