HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 27, 2016

Zantel yaleta Mtambo mpya ili kuboresha huduma ya Mawasiliano nchini

Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa-Baucha (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya kuwasili vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies. Akimsikiliza ni afisa wa Huawei William Cheng (Wei).
Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa (kulia) akifurahia jambo na maafisa waandamizi kutoka Zantel, Ericsson na Huawei, baada ya mkutano na waandishi wa habari kuelezea mtandao ulioboreshwa wa Zantel unaoanza kujengwa hivi karibuni. Mradi wa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu.
Alex Kamamia wa Ericsson (wa pili kulia) akielezea jinsi mtambo mpya wa mawasiliano ya Zantel utakavyoboresha huduma kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel. Wakimsikiliza ni Mkuu wa Ufundi wa Zantel Larry Arthur (kushoto) na Jx Chen wa Huawei (wa pili kushoto) na Frode Dyrdal (kulia) wa Ericsson.
Meneja Miradi wa Zantel Zanzibar Mohamed Ahmed Jaye, akielezea waandishi wa habari (hawapo pichani), jinsi mitambo mipya ya Zantel inavyofanya kazi. Zantel imeanza mradi mkubwa wa kuborersha mtandao wake nchi nzima kwa kufunga mitambo mipya ya mawasiliano kwa ushirikiano na Huawei Technologies na Ericsson.
Mkuu wa Ufundi wa Zantel Larry Arthur (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya kuwasili vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies. Kushoto ni William Cheng (Wei) kutoka Huawei, wa pili kushioto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa(Baucha), na kulia ni Frode Dyrdal wa Ericsson.
Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa (wa pili kulia) na Mkuu wa Ufundi wa Zantel Larry Arthur (wa pili kushoto), wakipongezana na wadau wao wakubwa katika uboreshaji wa mtandao za Zantel unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu ijayo. Kulia ni Frode Dyrdal wa Ericsson na kushoto ni William Cheng wa Huawei.
Baadhi ya vifaa vipya vilivyowasili Zanzibar kutoka kampuni za Ericsson na Huawei Technologies tayari kwa uboreshaji wa mtandao wa Zantel katika mradi wenye gharama ya zaidi ya Tsh. 2bn/- unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu. Baada ya kukamilika watuamiaji watapata mawasiliano yenye ubora zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad