HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 28, 2016

SSRA YAWAPA SOMO WANAHABARI JIJINI DAR LEO

 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akizungumza katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es salaam leo. Katika Semima hiyo, SSRA iliweza kuzungumzia namna inavyofanya shughuli zake za kuisimamia mifuko ya hifadhi za jamii. Wengine pichani ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde Msika (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini SSRA, Ansgar Mushi.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, katika semina ya siku moja iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Semina hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
 
Mwandishi wa habari kutoka Gazeti la The Citizen akiuliza swali.
Mwandishi wa habari kutoka Azam Media, Wasiwasi Mwabulambo akiuza swali.
Mwandishi wa habari wa TBC, Angela Msangi akiuliza swali.
 Picha ya pamoja.

1 comment:

  1. Toeni riba ili nikijachukua hela yangu nifaidike nayo kama ninyi mnavyofaidika ktk kuwekeza miradi yenu.siyomtu anaweka miaka kumi then anakuja kuchukua kiwango kile kile cha mwaka 47 wakati hata thamani inakua imeshuka. badirisheni mfumo hilo halikubariki.si bora nikaweke kwenye fixed deposit ambayo najua baada ya muda nitapata na interesty!??

    ReplyDelete

Post Bottom Ad