HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 30, 2016

NANI ZAIDI KATI YA YANGA NA SIMBA?

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHAMRA SHAMRA za mechi ya watani wa Jadi baina ya Yanga na Simba zinazidi kupamba moto kwa kila upande kujinadi kwa kila namna.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa saa 10, ukichezeshwa na Mshambuliaji wa beji ya FIFA, Martin Sanya akisaidiwa na Frank Chacha na Mpenzu huku mezani akiwa Hery Sasii.

Mechi hiyo itakayoanza kutumia mfumo mpya wa kadi za kieletroniki umekuwa na hamasa kubwa sana kwa mashabiki na wengi kujitokeza kuchukua kadi hizo.

Yanga wakiwa njiani kuingia Dar es salaam wakitokea Pemba walipoweka kambi ya wiki moja, Simba tayari wameingia jijini na asubuhi ya leo kufanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Gymkhana.

Timu hizi zimeweza kukutana mara 96 na tayari  Mabao  196 yakiwa yamefungwa huku katika mechi tano  tano za mwisho Yanga ameshinda mara mbili, Simba ikishinda mara moja na sare mbili. Yanga Ikiwa haijabadilisha benchi la ufundi  pamoja na kikosi kwa muda mrefu wanakutana na Simba ambayo imebadilisha asilimia kubwa ya wachezani na benchi la ufundi.

Lakini siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.

 Mbao na JKT Ruvu Jmwatakuwa  kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad