HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 27, 2016

MOROGORO KUANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO MKOANI HUMO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika Mkoani Morogoro Septemba 29-10, 2016 lenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, kwani umejaaliwa kuwa na mazingira mazuni na uwepo wa rasilimali nyingi ambazo bado hazitumika ipasavyo, pia amewataka vijana wa kitanzania kuacha kukimbilia mijini na badala yake wajikite kwenye fursa ya uwekezaji wa kilimo na ufugaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akifafanua jambo katika Mkutano huo na Waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji Mkoani Morogoro litakalofanyika Septemba 29-10, 2016 , ambapo amesema kuwa Kongamano hilo litasaidia kuutangaza Mkoa wa Morogoro kama miongoni mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa Makampuni ya ndani na nje ya nchi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe akimueleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari, wakati wa Mkutano huo na Waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji Mkoani Morogoro litakalofanyika Septemba 29-10, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad