HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 1, 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AJITAMBULISHA KWA VIONGOZI WA DINI MKOANI HUMO

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa Angela Kizigha.

Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao.

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
 
Gambo amekutana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.

Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.

Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali zitakazowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Amewataka wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.

Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Aidha alishauri kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
 
Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili watoe mawazo yao katika kuiboresha na kuifanya itekelezeke kwa wepesi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad