Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Boma Raballa na Mwenyekiti
wa Mashindano ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali, Michael Luwongo wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya
shilingi milioni 40 kwaajili ya kudhamini mashindano ya mkuu wa majeshi
yatakayofanyika Septemba 24 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Boma Raballa akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 40 Mwenyekiti wa Mashindano ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali, Michael Luwongo kwaajili ya kudhamini Mashindano ya Kikombe cha Mkuu wa Majeshi yatakayofanyika Septemba 24 mwaka huu katika viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Boma Raballa akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 40 kwaajili ya Kudhamini mashindano ya kikombe cha Mkuu wa Majeshi cha mchezo wa gofu kwaajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Jeshi katika Mchezo wa Gofu kwa klabu ya Mchezo huo Jeshini hapo jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya mchezo wa Gofu Lugalo. Kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali, Michael Luwongo.
No comments:
Post a Comment