HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 4, 2016

ENEO LA KARIAKOO KUWA MKOA MAALUMU WA KODI- TRA.


Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
ENEO la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu  wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini eneo hilo litasaidia kwa kila mfanyabiashara kuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa hiyo ni moja ya Mkakati wa harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka  inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka huu wa fedha.

Kayombo amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni  asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.

Pia Kayombo ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo TRA vilivyo karibu kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo.

Amesema kuwa vituo vya kuhakiki taarifa zao ni pamoja na vitua vya 
Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
Wilaya ya Kigamboni - Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji. 

Kayombo pia amewahimiza wamiliki wa vituo vya  mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga  mashine za EFDs kabla Septemba 30 mwaka huu  kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe Oktoba 1 na  hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Na walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo  wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kuhusiana na mikakati mbalimbali waliyojiwekea Mamlaka ya Mapato(TRA) ili kuhakikisha Mapato yanakusanywa ipasavyo.
Baadhi ya waandishi wa Habri wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad