HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 5, 2016

AUWSA YAJA NA RASIMU YA MABORESHO YA HUDUMA KWA MTEJA


Mgeni Rasmi ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Arusha.Afisa Tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutahengerwa akisoma hotuba hiyo mbele ya wadau wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha leo kushoto ni mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Auwsa Ruth Koya na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Auwsa Job Laizer na mjumbe wa bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye mkutano wa Maboresho ya rasimu ya mkataba wa huduma za mteja. Picha zote na Mahmoud Ahmad.
Mkurugenzi wa Auwsa Ruth Koya akiongea na kujibu maswali ya wadau wa mamlaka hiyo na wakazi wa jiji la Arusha juu ya maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja leo jijini Arusha.

Baadhi ya wadau na wakazi wa jiji la Arusha wakifuatilia majibu ya mkurugenzi juu ya uboreshaji wa huduma kwa mteja kwenye viwanja vya makumbusho jijini Arusha.Maafisa wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Mamlaka hiyo wakiwa wanaratibu shughuli hiyo kama walivyokuwatwa na kamera ya matukio ya michuzi blog jijini Arusha leo.
Maafisa wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wakiandika maelezo na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na wadau wa Auwsa pamoja na wakazi wa jiji la Arusha.
Wakazi mbali mbali wa jiji la Arusha walioshiriki mkutano huo wa maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja picha juu na chini.


Na Mahmoud Ahmad, Arusha

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiza imewataka wakazi wa jiji la Arusha kukaa mkao wa kula kwani wapo katika wakati wa kuboresha huduma zake kwenye kipindi cha miaka miwili na nusu iliyobakia katika uboresha wa miundombinu na utafutaji wa vyanzo vipya vya maji na kuwa tatizo la maji litakuwa historia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AUWSA Ruth Koya wakati akijibu maswali ya wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Mkutano wa maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja jijini Arusha.

Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya upungufu wa maji kwa mda mrefu na serikali imeliona hilo ndio maana ikatenga kiasi cha tsh,476 bilion za uboreshaji wa huduma mbali mbali za mamlaka hiyo hivyo suala hilo linafanyiwa kazi kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2018 litakapokamilika.

“Tuwe na subra maradi huu kwa sasa una mda wa miezi nane tangia uanze na mkandarasi wa utafutaji wa vyanzo vya maji yupo kazi akishakamilisha tutaanza maboresho ya miundombinu yetu ilkuweza kuwafikishia maji kwa wateja wetu wote”alisema Koya

Kwa upande wake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Afisa tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutehengerwa aliitaka Auwsa kuwabainisha wezi wote wa maji ilikuweza kuwafisha katika mikono ya kisheria kwani suala hilo pia linachangia wananchi kukosa huduma ya maji safi na upotevu wa maji.
 
Alisema kuwa kumekuwapo na vyanzo vingi vya maji zaidi ya 19 na vingine vimeanzishwa na viwanda ambavyo vimekuwa vikiikosesha Auwsa mapato ikiwemo kiwanda cha A to Z ambacho kimekuwa kikigawa maji bure huku wakitambua kuwa wao hawana mamlaka ya kisheria ya usimamizi wa maji hivyo ni mteja mkubwa mnampoteza kulipa huduma za maji.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Job Laizer alisema kuwa Malalamiko ambayo wananchi wameyatoa ni changamoto kubwa kwao katika kuifanya mamlaka hiyo kuboresha huduma zake na kuwaahidi wadau kuyasimamia na kuahkikisha wateja wanapata huduma bora na kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad