HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 24, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA ENEO LILILOTOKEA TUKIO LA MAUWAJI YA ASKARI POLISI HUKO MBAGARA, JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba usiku wa kuamkia leo, alifika eneo la Mbagara Mbande Wilayani Temeke, Jijini Dar es salaam na kujionea eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo inadaiwa kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha za vita, walivamia eneo la Benki ya CRDB - Mbande na kuwashambulia kwa risasi Askari waliokuwepo eneo hilo na kupekea vifo vya askari hao ambao walikuwa wanne wakati walipokuwa wakishuka  kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.

Waziri Nchemba pia aliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi ambao ni raia wa kawaida wawili, ambao hali zinaendelea vizuri.

Waziri Nchemba amelaani tukio hilo na matukio mengine kama haya, na kutoa rai kwa wahusika kujisalimisha wenyewe, na kuwaomba wananchi na raia wema kutoa ushirikiano wa kifichua waovu wa matukio ya namna hiyo na mengine mengi, ili kupambana na wahalifu hao wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, wakati walipokuwa eneo la tukio.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro wakionyesha maeneo mbali mbali ya Gari la Polisi lilivyoshambuliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimjulia hali mmoja wa Raia aliejeruhiwa katika tukio hilo.
Muonekano wa gari ya Polisi iliyokuwa ikitumiwa na Askari hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad