HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 28, 2016

SIKINDE NGOMA YA UKAE, COCODO NA THE SPIRITS BAND WALIVYOKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAO KATIKA TAMASHA LA WAZI LA MUZIKI JIJINI DAR

 Wanamuziki wa Bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae, wakiyarudi magoma katika Tamasha la wazi la Muziki lililofanyika kwenye Viwanja vya NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016. Tamasha hilo ni muendelezo wa matamasha ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika eneo hilo, huku hilo likiwa na upekee, kwani lilihusisha uzinduzi wa Nyimbo mpya mbali mbali za Bendi tatu tofauti ambazo ni Sikinde wenyewe, Cocodo pamoja na The Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani. Ilikuwa ni burudani ya aina yake yenye kuvutia wengi waliofika kwenye eneo hilo maarufu kwa kazi mbali mbali za Sanaa.
 Sikinde wakiendelea kulishambulia Jukwaa.
 Mdomo wa Bata ukipulizwa kwa ustadi wa hali ya juu na Mkongwe huyu wa Bendi ya Sikinde.
 Mcharaza gitaa katika umahiri wake.
Ukisikia muziki mzuri ikikatika katika masikio yako, basi jua kuna vyombo vingi sana vinavyopelekea muziki kuwa mzuri na moja ya hivyo ni hii midomo ya bata.
 Abdallah Hemba wa Sikinde Ngoma ya Ukae akiongoza mashambulizi ya Bendi yake hiyo kwa Mashabiki wao waliofurika kwa wingi kwenye Viwanja vya NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016.
 
Wanamuziki wa Bendi ya The Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani wakifanya yao jukwaani.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad