Gerson Partinus Msigwa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication -
DPC).
Taarifa
iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo
imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31
Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.
Kabla ya
uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus
Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika
Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.
Jaffar
Haniu
Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais
Msaidizi.
Dar es Salaam
31 Agosti, 2016
No comments:
Post a Comment