HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 29, 2016

WADAU WACHANGIA VITI NA MEZA KWA SHULE ZA SEKONDARI

Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipokea kiti toka kwa mwakilishi wa Sayona Fruits Ltd ya Mboga iliyo chini ya kampuni ya MMI Steel ya Jijini Dar es Salaam, Abubakary Mlawa wakati wa makabidhiano ya viti na meza 724 kwa Shule tano za Sekondari za Jimbo hilo zoezi hilo lilifanyika kwenye shule ya Sekondari ya Lugoba.

Mbunge waMbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipokea meza toka kwa mwakilishi wa Sayona Fruits Ltd ya Mboga iliyo chini ya kampuni ya MMI Steel ya Jijini Dar es Salaam, Abubakary Mlawa wakati wa makabidhiano ya viti na meza 724 kwa Shule tano za Sekondari za Jimbo hilo zoezi hilo lilifanyika kwenye shule ya Sekondari ya Lugoba.
Na John Gagarini, Chalinze

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amepokea viti na meza vyenye thamani ya shilingi milioni 80kutoka kiwanda cha Matunda cha Sayona Fruits Ltd kwa ajili ya shule za sekondari za Halmashauri ya Chalinze.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mbunge huyo na mwakilishi wa kampuni hiyo Abubakry Mlawa kwenye shule ya sekondari ya Lugoba na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maofisa toka Halmashauri hiyo.

Akiishukuru kampuni hiyo ya Sayona Ridhiwani amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwani wanaisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa madawati kwa wanafunzi.

Ridhiwani amesema kuwa wamefarijika kuona mchango huo ambao umekuja wakati mwafaka wa kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakisoma kwenye mazingira magumu kutokana na kutokuwa na madawati hali ambayo inwafanya washindwe kusoma vizuri.

Amesema kuwa walikuwa na uhaba wa vitina meza 724  kwa ajili ya shule tano ambapo zingine hazina tatizo la upungufu wa vifaa hivyo huku kwa shule za msingi upungufu ni madawati 1,500 ambapo wanatarajia kukamilisha upatikanaji kwani baadhi bado yanendelea kutengenezwa.

Aidha amesema kuwa Chalinze imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dk John Magufuli la kuhakikisha kuwa wanafunzi hawakai chini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye wilaya ya Bagamoyo.

Amebainisha kuwa changamoto ambayo inaibuka kwa sasa ni madawati kuwa mengi huku kukiwa na upungufu wa madarasa na hiyo imetokana na wanafunzi wengi kujiunga na shule kutokana na serikali kuweka mpango wa wanafunzi kusoma bure hivyo kufanya madarasa kujaa.

Amewataka wadau wengine nao kujitokeza ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo mapema iwezekanavyo na anaamini watafanikiwa kwani wameonyesha moyo wa kusaidia watoto wao waondokane na adha hiyo.

Kwa upande wake Abubakary Mlawa amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha wanafunzi kukaa kwa nafasi na kwa wale wa shule za msingi wasikae chini ili waweze kusoma vizuri.

Mlawa amesema wameshatoa madawati 600 kwa Halmashauri ya Bagamoyo na watatoa madawati 600 kwa Halmashauri ya Chalinze kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Amesema kuwa wao wako tayari kusaidia ujenzi wa madarasa mapya ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi ambao wamejitokeza kwa wingi kutokana na mpango huo wa serikali wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad