HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 27, 2016

VIBWEKA VYA KAMATI ZA UFUNDI KATIKA MASHINDANO YA NDONDO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UKITAKA kujua aina mbalimbali za vibweka vya kamati za ufundi katika michezo hasa ya soka, pamoja na aina mbalimbali za ushangiliaji basi fatilia mashindano ya Ndondo ambako ndio Mahala pake. Vibweka, vituko na kila aina ya ushangiliaji utauona hapo, Wapo wanaojipaka damu (za kuku), masizi ya mkaa, kujichora mwili mzima na hata wale wanaovaa tofauti na wengine. 

Raha ya Ndondo ni uipeleke kwenye viwanja ambavyo mashabiki wataweza kuonesha aina zao za ushangiliaji na hutataka kuamini dakika 90 zinamalizika mtu hajashuhudia hata dakika moja kwani muda wote anakuwa anafanya vibweka vinavyowaacha hoi mashabiki waliokuja kushangalia mchezo huo wa soka la mtaani maarufu kama Ndondo.

Katika uwanja wa Bandari 'Wembley'  unawapa nafasi mashabiki kufanya vituko vya kila aina na kufanya mchezo huo kugeuna ni sehemu ya burudani kwa washabiki wengine wa vibweka. 

Burudani ni kokote, kawaida ya viwanja hivi maeneo ya kukaa watu ni sehemu chache sana ila ukitaka kujua mchezo wa mpira utaona wakitumia kila aina ya njia ili kuweza kuuona. Juu ya miti, juu ya magari kote kunawezekana.
Hii ndiyo raha ya NDONDO.
Mtaalam wa Ufundi wa Timu ya Temeka Market akiwasili uwanjani huku akiwa na ulinzi wa nguvu.
Bendi toka Tandale ikitumbuiza wakati Timu yao ya Makumba FC ikikipiga. 
 Mtaalam akiwa tayari kwa kazi ya kuitafutia ushindi timu yake kutokea nje ya uwanja.
Jukwaa kuu. 
Mtaalam toka Timu ya Misosi FC akipelekwa uwanjani kwa mtindo wake.
Huyu dogo nae alikuwepo uwanjani kuisapoti timu ya Mshua wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad