HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 1, 2016

TPA YAKABIDHI MSAADA WA SH.MILIONI 250 KWA AJILI YA MADAWATI.

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipokea mfano wa hundi ya sh.miliioni 250, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya  Mamlaka ya  Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa  Ignas Rubaratuka. Fedha hizo ni kwaajili ya mchango wa madawati, Dar es Salaam leo. Wakwanza kulia ni  Mkurugenzi  Mkuu TPA, Mhandisi  Deusdetit  Kakoko. 
(Picha na Christopher  Lissa).

 Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa
Sh. milioni 250 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili 
ya kuchangia kampeni ya madawati Mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na tatizo la kukaa chini wanafunzi.

Licha ya kukabidhi msaada huo mamlaka hiyo pia imechangia kiasi cha Sh
milioni 165 katika Halmashauri 11 nchini zenye uhaba wa madawati ambazo walizianisha katika uhitaji wa msaada huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi (TPA) Profesa Ignas Rubaratuka alisema, msaad huo ni
kutekeleza jukumu katika kuunga mkono kampeni ya Rais katika
kuhakikisha wanatatua tatizo la ukosefu wa madawati katika Wilaya za
Mkoa huo ili watoto wa kitanzanbia wwasome katika mazingira bora.

“Pamoja na shughuli zake za kupakua na kupatia mizigo pia mamlaka
imekuwa mstari wa mbele kuchangia masuala ya kijamii kupitia sera yake
ya msaada kwa jamii (CSR) ambapo inashiriki kikamilifu kurudisha faida
yake kwa jamii,” alisema

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo Makonda ameishukuru mamlaka
hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia sekta ya elimu ambayo imekuwa
ikukabiliwa na changamoto kubwa hasa ya uhaba wa madawati.

Amesema msaada uliotolewa na TPA utasaidia kupunguza uhaba wa madawati 
zaidi ya laki nane unaolikumba jiji la Dar es Salaam ambao utasaidia 
kupunguza adha wanayoipata wanafunzi.

“Tunachangamoto kubwa ya madawati na tumeambiwa mpaka ifikapo juzi
tuwe tumekamilisha kampeni ya madawati najua Mkoa wangu ni miongoni
mwa mikoa yenye uhaba mkubwa lakini ninyi bado mmenipa nguvu ya
kuamini tutafanikiwa na kibarua changu kitaendelea kuwa salaama,”
alisema Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu TPA Deusdedit Kakoko alisema wameamua 
kutoa msaada lengo ni kurudisha kiasi kwa jamii na msaada uliotolewa 
umetolewa kwa makubaliano yao pamoja na wafanyakazi wa TPA ili kuondoa 
uhaba wa madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa mingine .

“Kampeni ya madawati mnayoifanya tunaiona na ndio maana tumeamua kutoa 
msaada huu kama mchango wa kampeni fedha zote tayati tumeshaweka 
katika akaunti za Mkoa naamini zitakwenda kufanya yale
yaliyokusudiwa,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad