HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 25, 2016

TEMEKE DERBY JULAI 30 NDONDO CUP

Mashabiki wakionesha namna mbalimbali za Ushangiliaji hapa kwa mtindo wa Yesu Msalabani mpaka dakika 90 zinamalizika katika mashindano ya Ndondo Cup yatakayofikia mwisho Julai 30 mwaka huu.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
UHONDO wa Ndondo twende ukaujue Julai 30, hapa Temeke Market hapa Kauzu Fc wote watoto wa Temeke wakitunishiana misuli wakitaka kumjua nani mbabe wa wilaya hiyo. 

Wakijivunia kulibakisha kombe ndani ya Temeke kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo.

 Ukiutaja uwanja wa Bandari watu wanaweza wakajiuliza ni upi huo ila almaarufu ni WEMBLEY walitumia jina la Uwanja uliopo nchini Uingereza. Katika uwanja huo unaobeba mashabiki zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja ukipewa sifa ya amani na utulivu kwa mashabiki.  

Hii ni fainali ya aina yake pale timu kutoka Temeke zikitambiana na kila mmoja na kujizatiti katika kulibakisha kombe hilo kwake, Kauzu Fc inakuwa ni fainali yao ya 2 mfululizo wakikumbuka machungu ya kunyang'anywa tonge na Faru Jeuri msimu uliopita.  Temeke Market ni mara ya kwanza kushiriki na kufanikiwa kuingia hatua ya fainali na kuweka rekodi kwa timu yao. Nani kuondoka nalo? Hilo litajulikana Wembley July 30.
Ukiachilia mbali ukubwa wa mashindano hayo kwa sasa, viongozi mbalimbali wameweza kujitokeza kwa wingi ambapo Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ameonesha kuvutiwa na mashindano hayo na kuwapa majukumu waandaji kuweza kuanzisha mengine kwa ajili ya shule za  sekondari. Katika fainali ya pili, Makonda aliweza kutoa ahadi ya 200,000 kwa golikipa wa timu itakayoingia fainali atazawadiwa huku aliyekuwa mbunge wa Tabora na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage dau lake lilishindwa kukamilika ila ameweza kuwakabidhi waandaaji kiasi cha shilingi 100,000 kwa ajili ya kupatiwa mchezaji atakayefunga goli la kwanza kwenye mchezo wa fainali.
Hivi kwani timu kubwa haziwezi kuja kuangalia vipaji huku mtaani ?? Swali hilo liliulizwa na Ismail Aden Rage(Pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Misosi FC na Kauzu FC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad