HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 28, 2016

PSPTB yahitimisha mafunzo kwa Wakurugenzi na wakuu wa Idara MNH

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa Lawrence Museru amewata Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Hospitali hiyo kuzingatia sheria ya manunuzi kama inavyoelekezwa .

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo ya siku tatu Profesa Museru amesema kila kiongozi wa MNH anapaswa kutambua umuhimu wa kuzingatia sheria hiyo ili kufanya kazi kwa weledi , kwani sheria hiyo si ya watu wa ugavi na manunuzi pekee.

“ Kila mmoja afanye kazi kama inavyotakiwa , tuwajibike na tufuate taratibu zote za manunuzi ni muhimu kuzingatia hilo ” amesema Profesa Museru.

Pamoja na mambo mengine Profesa Museru amewashukuru PSPTB kwa kutoa mafunzo hayo na kueleza kuwa lengo ni kila mmoja kuona umuhimu wa kuzingatia sheria ya manunuzi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Clemence Tesha amesema hii ni mara ya pili kwa PSPTB kutoa mafunzo hayo na kwamba wapo tayari kuendelea kutoa elimu kadiri inavyohitajika.

“ Tupo tayari kuendelea kuelimisha na kutoa mafunzo haya ili watumishi wafanye kazi kwa ufanisi zaidi” amesema Mkurugenzi Tesha.

Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yamefanyika MHN yalianza Julai 25 , 2016 na kuhitimishwa leo ambapo mada mbalimbali zimetolewa ikiwemo , Usahili na utaratibu, mpangilio wa taasisi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011.

Mada nyingine ni marekebisho ya sheria ya manunuzi ya mwaka 2016 , uandaaji wa hadidu rejea na mahitaji ya kitaalam, uandaaji wa nyaraka za zabuni , mapungufu katika uandaaji wa nyaraka za zabuni , kufanya tathimini na kulinganisha wazabuni, mapungufu katika kufanya tathimini na kulinganisha wazabuni pamoja na usimamizi wa mikataba.
Mtoa mada Kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania Meneja Manunuzi, Fredy Mbeyella akitoa mada katika mafunzo ya siku tatu juu ya sheria ya manunuzi, mafunzo hayo yametolewa kwa wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa siku tatu wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa .
Mkuu wa Idara ya watoto Dk. Mary Charles akipokea cheti cha kuhitimu ushiriki wa mafunzo hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- Lawrence Museru akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Bodi ya Wazabuni wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk . Faraja Chiwanga.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya dharura na ajali MNH Dk. Juma Mfinanga akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo ambayo yamehitimishwa leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Museru akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo ambayo yametolewa na PSPTB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad