HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 30, 2016

PICHA ZA MAPOKEZI YA MWILI WA HAYATI JOSEPH SENGA ALIEKUWA MPIGA PICHA MKUU WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA LEO


Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, Mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, na baadhi ya waaandishi na wapiga picha, leo wamejumuika pamoja kwenye kuupokea Mwili wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, wakati ulipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ukitokea nchini India. 
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa.
 Marehemu Senga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifa za ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA Khalfan Said/Othman Michuzi) .



Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili.
Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



 

Nikimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga.
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili.
Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo.
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo.
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
 Waombolezaji miongoni mwao wakiwemo waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa MpigaPicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaamm jana, ktuoka nchini India ambako alipatwa na mauti. Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia alifika kwenye mapokezi hayo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Senga wakiwa Uwanja wa Ndege wakisubiri wa mpendwa wao.
 Waombolezaji wakiuweka mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa Hos[pitali ya Muhimbili
 Wanachama wa Press Photographers Tanzania wakishiriki kuingiza kwenye gari jeneza la mwili wa wa aliyekuwa mpiga picha za habari Tanzania, marehemu Senga
 Dada wa marehemu Joseph Senga, Yunista Senga akilia kwa uchungu alipoona jeneza lenye mwili wa kakake, Joseph Senga

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akielezea kwa masikitiko kuhusu msiba wa Joseph Senga.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wapigapicha za habari wakiondoka Uwanja wa Ndege baada ya kuupokea mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad