HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 30, 2016

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYONOGA KATIKA FAINALI YA NDONDO CUP 2016, TEMEKE MATKET YATWAA UBINGWA

FAINALI ya Sports Extra Ndondo Cup imemalizika leo Jumamosi Julai 30, 2016 kwa timu ya Temeke Market kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kauzu FC mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Bandari (Wembly), Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo umeshuhudia timu ya Temeke Market ikiibuka mabingwa kwa kuwafunga Kauzu FC ambapo Mabao ya Temeke Market yalifungwa na Ramadhan Madebe, Shaban Kisiga na Adam Kingwande huku lile la Kauzu FC likifungwa na Rashid Tumbo.

Kwa kutwaa ubingwa huo Temeke Market wamejitwalia kombe pamoja na shilingi milioni 10 huku wakitoa mchezaji bora wa mashindano hayo ambaye Shaban Kisiga aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja, viatu na tuzo.

Kisiga amesema kuwa anafurahi kuona kuwa amekuwa mchezaji bora kwa mara ya pili mfululizo na ametaka waandaaji wa mashindano haya waboreshe zaidi ikiwemo kukarabati viwanja vitajavyotumika. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mgeni Rasmi katika Fainali hiyo, alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (katikati) alieambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine. Pichani ni Timu iliyoshika nafasi ya pili ikipita kukabidhiwa zawadi yao ikiwa ni mfano wa hundi yenye kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwa Kampuni ya Simu ya Airatel Tanzania, iliyokabidhiwa na Meneja Mawasiliano wake, Jackson Mmbando.
Mchezaji wa Temeke Market akiwania Mpira wa Juu mbele ya Beki wa Kauzu FC.
 
Mambo yalivyokuwa baada ya kuruka.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwasili uwanjani hapo.
Nyanda wa Timu ya Kauzu FC akiondoa hatari iliyoelekezwa langoni kwake katika Mtanange wa Fainali kati ya Timu hiyo na Temeke Market iliyoibuka na Ubingwa wa Mashindano ya Ndondo Cup 2016.
Temeka Market wakijipatia Bao la tatu.
Mshabiki wa Temeke Market akionyesha furaha yake.
Kipa wa Kauzu akizuiliwa na Wachezaji wenzake wakati alipokwenda kumzonda Mwamuzi wa Mchezo huo.
Kipa wa Temeke Market akionyesha uwepo wake mbele ya Washambuliaji wa Kauzu FC.
Nahodha wa Timu ya Kauzu FC, Godfrey Taita akiondosha hatari upande wao.
Kauzu Wakijipatia Bao la kufutia Machozi.





Meza Kuu.

Mtu wa Huduma ya kwanza akitoka kumuhudumia Mchezaji.
Chifu wa Kauzu FC akiwa haamili kilichotokea Uwanjani hapo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad