HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 27, 2016

GONZALO HIGUAIN ATUA JUVENTUS KWA DAU LA PAUNDI 77.3 MIL

Na Dac Popos
Suala la kutumia fedha nyingi za uhamisho kwa wachezaji wa kandanda hasa barani Ulaya linazidi kushika kasi ambapo klabu ya Juventus (vibibi kizee wa Turin) walipo msajili mshambulizi mahiri wa timu ya As Napoli raia wa Argentina Gonzalo Higuain, kwa kitita cha Pound milioni 77.3.

Higuain ambaye alijiunga na Napoli toka Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 34-5 mwaka 2013, anakuwa mchezaji wa tatu duniani kuhamishwa kwa kiasi kikubwa cha pesa nyuma ya Gareth Bale anaye ongoza kwa uhamisho uliofikia Pound milioni 85 toka Tottenham kwenda Real Madrid na Christian Ronaldo toka Manchester United kwenda pia Real Madrid kwa Pound milioni 80.

Hata hivyo imebainika kwamba malipo hayo hayatolipwa yote kwa mkupuo bali yatalipwa kwa awamu mbili.

Higuain ambaye alianza kujulikana kisoka alipokuwa akiichezea timu ya River Plate ya nchini kwao Argentina ameshinda kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa ligi ya Italia Serie A almaarufu kama CAPOCANNONIERE akiwa amefunga magoli 36 na kuisaidia Napoli kushika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Juventus. Hii ni mara ya pili katika karne hii kwa mchezaji mmoja kufikisha idadi ya mabao zaidi ya 30 kwenye serie A, mchezaji wa kwanza alikuwa ni Luca Toni.

aliyefunga magoli 31 akiwa na timu ya Fiorentina msimu wa 2005-06.



Wakati hayo yakijiri Italia, huko Marekani kocha wa timu ya Liverpool (Majogoo wa jiji) Jurgen Klopp amemrudisha Uingereza beki wake kisiki Mamadou Sakho toka kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huko Marekani.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu za kurudishwa huko kwa beki huyo, ingawa taarifa nyingine zikidai kuwa amerudishwa ili akapate matibabu ya mguu ambao huwa unamsumbua, na taarifa nyingine zinadai karudishwa kutokana na nidhamu mbovu aliyoonesha.Vitendo vya nidhamu mbovu vinavyodaiwa kuonyeshwa juu yake kwanza ni tukio la yeye Sakho kuchelewa kufika uwanja wa ndege wakati wakielekea USA, na jingine ni kuuingilia mahojiano ya kocha na waandishi wa habari.
Sakho mwenye umri wa miaka 26 ambaye hivi karibuni alishinda kesi ya kuhusika kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni baada ya kutumikia adhabu ya kufungiwa kwa siku 30 na kusababisha akose kushiriki michuano ya Euro 2016, alijiunga na Majogoo hao kwa dau la Pound Milioni 18 akitokea Paris St-Germain mwaka 2013 na amecheza michezo 55 na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad