HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2016

WAENDESHA BODABODA 35 KUPANDISHWA MAHAKAMANI TEMEKE.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Mkoa wa Temeke linawashikilia waendesha bodaboda 35 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutovaa kofia ngumu (Helmet).

Akizungumza na  Repota wa Globu ya Jamii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,  Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi  (ACP), Gilles Muroto amesema kuwa kukamatwa kwa bodaboda hao kumetokana na opresheni wanayoifanya ya usalama barabarani ambayo ni endelevu.

Amesema  kuwa  wanawasiliana na mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) juu ya kuweza kuwafikisha mahakamani waendesha bodaboda kwa makosa ambayo wanahusika nayo.
‘’Temeke tumejipanga kuhakikisha kila mtu anayetumia chombo cha moto anafuata sheria na kanuni  na wataokwenda tofauti watafikishwa katika vyombo vya sheria’’Amesema Muroto.

Aidha amesema kuwa opresheni hiyo ni endelevu haishi leo hivyo wale ambao wanajua zimamoto wakikamatwa na makosa ambayo wanapigiwa kelele ikiwa ni usalama wao.

Muroto amesema ametaka wananchi kutoa ushirikiano wa vitendo vya kialifu ili kuweza  jeshi kufanya kazi yake na kuweza kuwakamata wale ambao wanajihusisha na uhalifu mbalimbali ndani ya Temeke.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad